Katika jaribio hili rahisi, tutauliza maswali machache kuhusu kile ambacho Biblia inasema kuhusu kunena kwa lugha. Majibu yako wazi sana hivi kwamba hatutayatoa hata kidogo. FIKIRIA kuhusu majibu hayo.
- Yesu alisema tutawatambua kwa (matunda, karama) yao.
- Tunahimizwa kujazwa na Roho, tukizungumza sisi kwa sisi kwa (lugha, zaburi na nyimbo na tenzi za rohoni).
- Lugha ni ishara (kwa mwamini, kwa asiyeamini).
- Paulo alipouliza swali “Je, wote hunena kwa lugha?” jibu lililoashiriwa lilikuwa (ndiyo, hapana).
- Wasioamini katika Matendo 2 (walihitaji mkalimani, hawakuhitaji mkalimani) ili kuelewa yale ambayo walionena kwa lugha walikuwa wakisema.


